Huu ndio ujio mwingine wa “Kidoti”


Ni time sasa ya wabongo kuanza kusapoti vitu vizuri vya kwetu na kuvikuza iliviweze kufika mbali, mrembo anayefanya mambo mengi sana ya kimaendeleo katika jamii, namzungumzia Jokate Mwegelo ameleta fashion yake ya mabegi ya mgongoni ambayo yamepewa chapa ya Kidoti.

Jokate anazidi kuonyesha kwamba Mwanamke katika jamii naye anaweza kufanikiwa kama ukiwa na akili, ujasiri na dhamira ya kufanya jambo fulani, baada ya kufanya vizuri na Chapa ya Kidoti kwa kuleta nywele zenye mitindo mbalimbali kwa ajili ya wanawake ambao wanapenda kupendeza bila kufilisi mifuko yao, huu ndio ujiomwingine wa “Kidoti” kwa kuleta mabegi ya mgongoni.


Kupitia kurasa yake ya Instagram amekuwa akiposti picha tofautitofauti zikionyesha fashion yake ya mabegi ya “Kidoti”, na jingine zuri la kufahamu ni kwamba katika mabegi hayo pia yametolewa special edition ambayo yatakuwa yakitoa ujumbe kwa watoto pamoja na vijana kujifahamu wao ni nani katika jamii.


No comments:

Drop your comment about this..