Susumila Ashtakiwa Tena

Msanii ambaye anatamba kwa wimbo wake mpya wa NGOMA IMEZIMA kwa mara nyengine tena amejipata ameshtakiwa. Mwezi uliopita, Susumila alishtakiwa na Kibibi Salim baada ya kutalakiana naye akihitaji kuhakikishiwa ya kwamba msanii huyo atakua anagharamia malezi ya mtoto wake namatumizi na mtalaka wake huyo kwa mda wa miezi mitatu kulingana na sheria za kiislamu. Ruth Jimmy ambaye ndio ‘baby mama’ wake wa kwanza kabla Kibibi naye amempeleka Susumila kortini akitaka msanii huyo awajibike katika malezi ya watoto wao wawili ambao wanaishi na mamayao. Kulingana na Ruth, Susumila amewatekeleza watoto wake kwani hajukumiki na mahitaji ya watoto wake kwa takriban mwaka mmoja sasa. Nilipomuuliza Susumila kama iwapo madai hayo yakutelekeza watoto ni ya ukweli alisema ya kwamba swala hilo la ulezi wa watoto ataliongelea kortini ila si kwa vyombo vya habari. NB:kupigia kura blog hii katika PwaniCelebrityAwards2016, tuma ujumbe wa neno 24C kwa 21195.


No comments:

Drop your comment about this..