Juma Nature: Kuna Watu Wanahonga Ili Ngoma Zangu Zisipigwe

Ukizungungumzia historia ya muziki wa Bongo Flava, haiwezi kukamilika bila kulitaja jina la mkongwe Juma Kassim Nature aliyewahi kutamba ngoma kama ‘Jinsi Kijana’, ‘Hili Game’ na zingine kibao. Hatimaye mkongwe huyo amaibuka na kudai kuwa kuna watu wanahonga ili nyimbo zake na za TMK Halisi zisichezwe redioni. Nature amesema kuwa miongoni mwa watu hao ni uongozi wake wa zamani lakini hakuwa tayari kuwataja kwa majina. “Sasa hivi kuna urasimu, kuna watu wanaenda kuhonga nyimbo zangu zisipigwe za Halisi zisipigwe, wapo watu wanafanya issue kama hizo na tayari tumeshaingia in deep kujua nini tatizo kwanini nyimbo hazichezwi,” ameniambia Nature nilipozungungumza naye nyumbani kwake Temeke. Ikumbukwe Nature alikuwa akifanya kazi chini ya kundi la Wanaume Family kundi linalomilikiwa na Said Fella kabla ya kujitoa kwenye kundi na baadhi ya wasanii wengine waliokuwa kwenye kundi hilo na kuanzisha kundi lao jipya linalofahamika kama Wanaume Halisi.


No comments:

Drop your comment about this..